Jumatatu, 26 Desemba 2016

KATIBA YA KANISA



YALIYOMO


                       
1.1. JINA LA HUDUMA
       Jina la huduma litakuwa “MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA”

      Anuani ya huduma itakuwa
      MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA
      S.L.P 131.
      HANDENI
      TANGA
      TANZANIA.

       Makao makuu ya huduma hii yatakuwa
       HANDENI  - TANGA -  TANZANIA.


Tamko la Imani, kwa mwafaka na waumini wa agizo la agano ( jipya) tunafungamana
na  azimio la tamko tuliaminilo yaani msingi wa Imani.(Yohana  3:16 )
Tukiombea kuwa kusiwe na madhara wala mgawanyiko tofauti, na kudhuru   amani miongoni mwa Huduma ndani na nje ya nchi yamkini sote tudumu kwa haja moja, kwa upendo mmoja kwa MUNGU mmoja mwenye enzi katika Imani zifuatazo:
(1Timotheo2:1-4.)
(a)       Tunaamini kwamba Biblia ni kitabu kitakatifu chenye sehemu mbili yaani Agano la              Kale lenye                    vitabu 27 na Agano jipya lenye vitabu 39 ni neno lenye pumzi ya Mungu.Tunaifanya           Biblia kuwa na mamlaka ya mwisho kuhusiana na Tabia ya Mkiristo.
            (2 Timotheo 3:16).

(b)     Tuna amini kwamba kuna MUNGU mmoja wa kweli, muumba wa mbingu na nchi na             Yeso Kristo                   ni mwana wake na Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu (1Yohana5:8-9).
             (c)       Tunaamini katika wokovu kwamba mwanadamu anaweza kupokea wokovu kwa                                        njia ya Imani kwa kumuamini Mwana wa MUNGU YESU Kristo kupitia kazi nzito aliyoifanya                pale Msalabani kwa msaada wa Roho Mtakatifu ( Warumi 10:9 ).

(d)   (i)     Tunaamini kwamba Kanisa la kweli hujengwa chini ya Msingi wa Yesu                                         Kristo ( 1 Wakorintho 3:11, Waefeso 2:20).
       (ii)    Tunaamini kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo
              (Warumi 12:5,Wakorintho12:2-15).na
       (iii)   Tunaamini kwamba Kristo ni kichwa cha Kanisa
              (Waefeso 5:23,Wakorintho11:3)

            (e)           Tunaamini katika ubatizo wa maji mengi. Ubatizo wa maji mengi ni amri ambayo kila                                 anayemwamini YESU ni lazima aitimize Amri hiyo. YESU Kristo alituamuru tubatizwe                                 katika maji mengi.(Yohana 3:22-23, Warumi: 6:3-9).

(f)      Tunaamini katika ubatizo wa Roho Mtakatifu. Ujazo wa Roho Mtakatifu ni ahadi kwa kila      mwamini ili kumwezesha mwamini kumtumikia MUNGU kwa Maombi na Kuabudu      katika               Roho Mtakatifu (Matendo 2:4-11, Warumi 8:26, Waefeso 6:18).

(g)        Tunaamini katika huduma 5  yaani Mitume, Manabíi, Wainjilisti, Wachungaji na Walimu.                  (Waefeso 4:11-12).

(h)       Tunaamini ndoa ya mume na mke mmoja katika Kristo Bwana (Mathayo 19:3-

            2.0. MALENGO NA MADHUMUNI YA HUDUMA:
            Malengo na Madhumuni ya HUDUMA ni kama ifuatavyo:

(a)        Kutekeleza kiutendaji agizo la kupeleka na kusambaza Injili kamili ndani na nje ya             nchi.

(b)        Kufuata mwangozo wa Roho Mtakatifu na kuandaa mfumo mzuri wa ushirikiano usio wa    ubinafsi, na wenye maisha Matakatifu kwa utendaji fanisi wa kazi ya MUNGU.

(c)        Kutoa uhuru wa kweli wa kuabudu na kutoa mafundisho thabiti katika Huduma na Washirika.

(d)        Kudumisha na kuleta ushirikiano na Huduma nyingine za kiroho.

(e)        Kutoa Huduma mbalimbali za Kiroho na Kimwili katika Jamii.

             Kwa mfano:
            Kiroho: Kufanya Semina na Mikutano ya Injili, Kuombea wagonjwa na                       
                          kuwapa Ushauri kwa ridhaa yao mahospitalini, mashuleni, 
                          magerezani na katika kaya.
           
             Kimwili:-
                        Kujenga na kuendesha shule, Zahanati, Hospitali, na Karakana za                                                             ufundi, uchapishaji na Studio za kureckodi uimbaji.

                         Nazo ni:-





          nazitakazowekwa.


3.4.1.   Ana haki ya kupata huduma  zote za kiroho na za kimwili  kulingana na mazingira yake ya                        kazi (mfano chakula, mahali pakuishi na matibabu yake) siyo malipo au mshahara.


             na pia makao makuu ita husika kumsaidia.




           yeyote yule.

                                                                      







                 Na HUDUMA. 

        
          AINA ZA WASHIRIKA
           Kutakuwepo na aina mbili za Washiriki nazo ni:
                                   
   3.6.1. Washirika  waanzilishi:
            Washirika hawa ndio walioshiriki katika kuandaa katiba hii.

     3.6.1.Washirika wapya:
            Washiriki wapya wa huduma hii wataendelea kupatikana kutokana na Mikutano ya             Injili,Semina, Makongamano na Maombezi ya wagonjwa yatakayofanyika          pamoja
             na wenye shida mbalimbali.      

            (i) Awe ameokoka
            (ii)  Awe amebatizwa katika maji mengi
            (iii)  Awe anashiriki katika Ibada na semina za Kiroho
            (iv)  Awe mwaminifu na mkwel kwa Mungu na kwa jamii.i
            (v)  Awe anashiriki katika shughuli za Huduma kwa kufuata taratibu                                                    zilizowekwa na zitakazo wekwa.

                        (i)    Kutekeleza maamuzi yote halali yatakayopangwa na HUDUMA kwa faida ya HUDUMA.
                        (ii)   Kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za HUDUMA.
                        (iii)  Kutoa ushauri utakaosaidia, kuimarisha na kuendeleza malengo ya           
                                  HUDUMA.

                        (i)  Anahaki ya kupata huduma zote za Kiroho mfano maombi, huduma 
                                za ndoa, mazishi, ugonjwa, ushauri nasaha na unasihi.
                        (ii)  Anahaki ya kuhoji anapoona dalili za ubadhilifu wa mali za HUDUMA.
                        (iii)  Hana haki ya kudai kurudishiwa michango ya aina yoyote aliyotoa                                                              kwa hiari yake mwenyewe kwa ajili ya shughuli mbalimbali za                                                                         maendeleo ya HUDUMA.
                        (iv)  Anao uamuzi wa kuendelea au kutoendelea na huduma bila kubughuziwa na                                                                           mtu yoyote yule.
                           (v)  Ana haki ya kuilinda na kuitetea misingi ya imani ya Kikristo.


           Kikomo cha mshirika katika HUDUMA kitasababishwa na :-
                       (i)  Kufukuzwa kwa kushindwa kufuata kanuni za Imani, Taratibu na  Sheria zilizowekwa na                                HUDUMA.
                       (ii)  Anapoamua kuacha kuwa Mshirika kwa hiari yake mwenyewe.

                             Muundo wa serikali kuu ya HUDUMA itakuwa kama ifuatavyo:
                             Kutakuwa na:-
                               (i)   Mwangalizi Mkuu.
                               (ii)   Katibu Mkuu.
                               (iii)   Mweka Hazina.
                               (iv)   Wangalizi wa Kanda
                               (v)    Wangalizi wa Majimbo.
                               (vi)   Wasimamizi wa Vituo vya HUDUMA
                              (vii)  Wazee na Watumishi wa Vituo vya  HUDUMA.

                                  Ni mwiko kwa Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa kutumia madaraka aliyopewa kwa                             ajili ya manufaa yake binafsi au kuwa na upendeleo wa namna yoyote ambao ni                                     kinyume na zilizowekwa.

                                Katika uchaguzi wowote ule kiongozi atakuwa ni yule atakayepata zaidi ya nusu ya kura                           zote zilizopigwa na wajumbe wanao husika waliohudhuria katika uchaguzi huo.

            Kutakuwa na Baraza kuu la Serikali ya HUDUMA. Baraza hilo litaundwa na Wajumbe wafuatao.
        4.2.1. Kamati kuu Tendaji.
        4.2.3. Baraza la Waangalizi wa Kanda na Majimbo.
        4.2.4. Wasimamizi wa Vituo vyote vya HUDUMA katika majimbo.
        4.2.5. WazeeViongozi  wa Vituo vya HUDUMA katika majimbo
        4.2.6 Wakuu wa Idara zote katika HUDUMA
        4.2.7. Wajumbe waalikwa / wataalamu.

          Baraza kuu litakuwa na kazi zifuatazo:
                     4.3.1. Litakuwa na mamlaka ya kuteua, kuchagua, kusimika, kusimamia utendaji kazi na                                    kutengua nyadhifa zao itakapo bidi.
                     4.3.2.  Litasimamia shughuli zote za HUDUMA.
                      4.3.3. Litasimamia maadili ya watumishi wote wa HUDUMA kwa ujumla.
                      4.3.4. Baraza kuu litakutana mara moja kila mwaka kati ya mwezi Desemba na Januari                                                             na maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.
                      4.3.5.  Litasimamia mali zote
                     4.3.6.  Kurekebisha katiba ya huduma itakapohitajika kufanyiwa marekebisho.
                      4.3.7.  Kupitisha taarifa za maendeleo ya huduma na kutoa mwongozo mpya.
                       
           Wafuatao watakuwa ni Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji:
                      4.4.1.  Mwangalizi Mkuu wa HUDUMA.
                      4.4.2.  Katibu Mkuu.
                      4.4.3.  Mtunza Hazina.
                      4.4.5.  Wangalizi wa Kanda.
                      4.4.6.  Wazee wa HUDUMA 2 wateuliwa.
                       
          Majukumu ya Kamati Kuu Tendaji yatakuwa kama ifuatavyo:
           4.5.1. Itafanya na kusimamia shughuli za kila siku za utendaji wa 
                      HUDUMA.
           4.5.2. Itatoa mapendekezo yatakayo jadiliwa na kupitishwa na Mkutano wa 
                       Baraza kuu.
           4.5.3. Hakuna kikao cha Kamati Kuu Tendaji kitakachofanywa bila
                                    kuwepo na koramu ya wajumbe wapatao theluthi mbili( 2/3).
                        4.5.6. Kurekebisha katiba ya huduma itakayo hitajika kufanyiwa                                                                          marekebisho
                        4.5.7. Kupitia taarifa za maendeleo ya huduma na kutoa miongozo mipya.
                       
       Mwangalizi Mkuu Atachaguliwa na Baraza kuu la Waangalizi.

          Majukumu ya Mwangalizi Mkuu yatakuwa kama ifuatavyo:-
                          5.1.1. Atakuwa na mamlaka ya kuangalia kazi zote za HUDUMA Kitaifa.
                          5.1.2. Atawajibika kufuatilia utendaji wa kazi wa Wangalizi wote walioko chini yake.
                          5.1.3. Atakuwa mwenyekiti wa Mikutano yote ya Baraza kuu na Kamati Tendaji.

                         5.2.1. Awe na Ujuzi katika Shughuli zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
                         5.2.2. Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.
                         5.2.3. Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau cheti)
                         5.2.4. Awe mtu asiyelaumika katika Jamii(Timotheo3:1-7)
                         5.2.5.  Awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza kwa lugha fasaha yaani Kiswahili,                                                   Kiingereza.

                         5.3.1. Katibu Mkuu atapendekezwa na Kamati Kuu Tendaji na atapitishwa na Baraza                                                                      kuu.
                         5.3.2.  Atakuwa katika Utumishi huu kwa muda wa miaka 5.
                         5.3.3. Kulingana na uwezo wake wa utendaji anaweza kuteuliwa tena.

                         5.4.1.   Awe na ujuzi wa kazi zitakazofanywa na HUDUMA  si chini ya miaka 5.
                         5.4.2   Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea

                         5.4.3. Awe na Elimu ya chuo cha Biblia (angalau cheti)




5.5.0. MAJUKUMU YA KATIBU MKUU:
                         5.5.1.  Atawajibika katika Utawala na Kuendesha Kazi za HUDUMA chini ya Usimamizi                                          wa Mwangalizi Mkuu
                         5.6.2. Atatunza kumbukumbu zote za Wasimamizi wa Vituo vya HUDUMA na taarifa                                                                       zote za Uongozi.
                         5. 5.3. Atakuwa katibu katika vikao / mikutano yote ya Baraza kuu na Kamati utendaji


                          5.6.1. Mtunza Hazina atapendekezwa na Kamati Kuu Tendaji na atapitishwa na                                                                                Baraza kuu.
                          5.6.2  Atakuwa katika Utumishi huu kwa muda wa miaka 5.
                          5.6.3  Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu wake katika HUDUMA anaweza                                              kuteuliwa tena.
                       
                          5.7.1.  Awe Mshirika wa Huduma.
                          5.7.2.  Awe na Elimu ya Kidato cha 4 na kuendelea.
                          5.7.3.  Awe na Taaluma ya Uhasibu.
                          5.7.4.  Awe mwaminifu na aliyejitoa kikamilifu kwa MUNGU.

                          5.8.1.  Atawajibika katika utunzaji na ukaguzi wa mali na fedha zote za Huduma.
                          5.8.2. Atatayarisha Taarifa ya Fedha, Mapato na Matumizi na kuwasilisha mbele ya                                              Baraza Kuu.
                          5.8.3. Atatekeleza kazi zake kwa kushirikiana na viongozi wake pamoja na Watumishi                                                                   wengine wa HUDUMA hasa Mwangalizi Mkuu na Katibu Mkuu.
                       
       Mwangalizi wa Kanda atachaguliwa na waangalizi wa Majimbo wa kanda husika na kithibitishwa
       na Baraza kuu.
                       
                           6.1.1. Awe na Ujuzi katika Shughuli zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
                           6.1.2. Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.
                           6.1.3.  Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau cheti)
                           6.1.4.  Awe mtu asiyelaumika katika Jamii(Timoteo 3:1-7)
                           6.1.5.  Awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza kwa lugha fasaha yaani Kiswahili,                                                                                      Kiingereza.
                            Kulingana na uweza wa utendaji na uaminifu wake katika HUDUMA anweza kuteuliwa tena.

                           6.2.1  Atawajibika kihuduma katika maeneo yote ya Kanda yake.
                           6.2.2.  Atawajibika kufuatilia utendaji wa kazi ya Mungu katika majimbo ya kanda  yake.
                           6.2.3. Atakuwa mwenyekiti wa mikutano na vikao vyote vya majimbo yake.





6.3.0. UTEUZI WA MWAGALIZI WA JIMBO/WILAYA:

                          6.3.1.  Mwangalizi wa Jimbo/Wilaya  atachaguliwa na Kamati Tendaji na              
                                     Kuthibitishwa na Baraza kuu
                          6.3.2.  Atatumika chini ya usimamizi wa mwangalizi wa kanda
                          6.3.3.  Kipindi cha utumishi kitakuwa miaka 5.
                          6.3.4.  Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu wake katika HUDUMA anaweza
                                     kuteuliwa tena
      
                        6.4.1.  Awe na Ujuzi katika Shughuli zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
                        6.4.2.  Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.
                        6.4.3.  Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau cheti)
                        6.4.4.  Awe mtu asiyelaumika katika Jamii (Timotheo3:1-7)
                        6.4.5. Awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza kwa lugha fasaha yaani  Kiswahili,                                                                        Kiingereza.

                      6.5.1. Atawajibika kihuduma katika maeneo yote ya Jimbo / Wilaya yake.
                      6.5.2. Atawajibika kufuatilia utendaji wa kazi ya Mungu katika makanisa yaliyo ndani ya jimbo                                         lake / wilaya.
                     6.5.3.  Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu wake katika HUDUMA anaweza  
                                kuteuliwa tena.
                                   
                    6.6.1. Msimamizi  wa kituo cha HUDUMA atateuliwa kulingana na Wito na Vipawa vya                                                  MUNGU vilivyo ndani mwake na kuthibitishwa na Mwangalizi Mkuu.
                    6.6.2. Msimamizi wa Kituo Cha HUDUMA atatumika chini ya usimamizi wa Mwangalizi                                      wa Majimbo/Wilaya.


                   6.7.1.  Atawajibika kihuduma katika Kituo cha HUDUMA anacho kiongoza kwa heshma  na                                   utumishi wake mzuri.
                    6.7.2.  Atapaswa apewe heshima sawa sawa na huduma ya kazi yake.
                    6.7.3.  Atateua viongozi katika Kituo chake, kuwasimika na kutengua nyadhifa  zao itakapo bidi.
                     6.7.4.  Atawajibika kulea vipawa mbalimbali vitakavyo ibuka katika Kituo Chake
                     6.7.5. Anatakiwa awe na uwezo wa kuongoza Washirika. (Ezekieli 23:4, 6, 15, 34:1-3, Matendo                                       20:28, Yohana21:15-17,1Petro 5:1-2)
                     6.7.6. Anapaswa awe mtumishi mkweli  na mwaminifu kwa MUNGU na kwa jamii.
                     6.7.7. Anao wajibu wa kulinda na kutunza mali za Kituo cha HUDUMA anacho kiongoza.
                       
Washirika wote wa HUDUMA hii wanawajibika kwa kuzingatia Mwongozo na sheria, pia kuwa           
na nidhamu, yamkini wanastahili adhabu wakifanya uhalifu wowote ule.    





Wazee na Wasimamizi wasaidizi wa Kituo cha HUDUMA - Watateuliwa na kusimikwa na Msimamizi   wa kituo cha HUDUMA. na watatumika chini ya uongozi wake.
                       
               8.1.1. Awe ameokoka.
               8.1.2. Awe amebatizwa katika maji mengi.
               8.1.3. Awe mwaminifu na mkweli kwa Mungu na kwa jamii.

              8.2.1. Wanawajibika kumsaidia MSIMAMIZI WA KITUO CHA HUDUMA
               8.2.2. Kutoa ushauri kwa msimamizi wa kituo na washarika kwa ujumla.

8.3.0. IDARA ZA HUDUMA:
                8.3.1. Idara ya Uinjilisti.
                8.3.2. Idara ya Vijana
                8.3.3. Idara ya Muziki
                8.3.6. Idara ya Wanawake na Watoto.
                8.3.7. Idara ya Akinababa.

             Idara zote katika kila kituo cha HUDUMA zitateuliwa na MSIMAMIZI WA KITUO CHA HUDUMA                          HUSIKA.
             Kipindi cha huduma kitakuwa ni miaka mitatu ( 3 ).baada ya hapo wakiwa            hawana lawama
             zozote  wanaweza kuendelea tena kipindi kingine.

8.4.0. VIONGOZI WASAIDIZI:


           Baraza kuu litakutana mara moja kila mwaka kati ya mwezi  Desemba na Januari.

8.7.0.   MKUTANO WA WASHIRIKA WOTE.
           

                          Kutokana na miradi mbalimbali / shughuli za kuogeza kipato.
                8.8.2. MATOLEO
                         Kutakuwa na matoleo ya aina mbalimbali, mfano sadaka za hiari, minada ya vitu mbalimbali                      na harambee.
                                   
            Kutakuwa na miradi mbalimbali ya HUDUMA
             Mfano: KILIMO, KARAKANA, STUDIO, VITUO VYA REDIO, SHULE, TV,USAFIRI,HOSPITALI,            UCHAPAJI NA UUZAJI VITABU.
8.8.4. MATUMIZI, UHASIBU NA UKAGUZI
Mapato yote yatakayopatikana yatatumika katika shughuli za maendeleo ya  HUDUMA    yakifuata   taratibu zote za kiuhasibu, lengo likiwa ni kufanikisha kuipeleka Injili ya BWANA katika Nchi yote ya Tanzania na nchi nyingine pia. Aidha sehemu ya mapato itatumika kutoa huduma ya kiroho na za kimwili katika jamii.
             Mfano:-  Kutoa huduma za kuwatunza yatima, wajane na masikini.

            Baraza la wadhamini litateuliwa na baraza kuu. Wajumbe wake hawatakuwa zaidi ya 5 na si chini   ya         watatu. Hawa watawajibika kulinda mali zote za HUDUMA.
            Huduma ya mdhamini itaisha endapo kutatokea:
9.1   Kifo
9.2  Kujiuzulu
9.3  Kura ya kutokuwa na Imani na mjumbe kutokana na mkutano wa wadhamini.
9.4  Mdhamini atatumikia wadhifa huu katika kipindi cha miaka 5.
9.5  Vikao vya wadhamini vitaendeshwa kwa kura ya wingi wa korumu isiyopungua wajumbe 3.
       Baraza la wadhamini litakutana mara mbili kwa mwaka.

            Kipengele hiki kimewekwa ili kurekebisha au kupendekeza marekebisho ya kanuni ama  
             sheria ya katiba hii. Pendekezo la marekebisho litafikishwa kwenye baraza kuu kwa uthibitisho.

            Katiba inaweza kufanyiwa marekebisho kwa Koramu ya theluthi mbili 2/3 za wingi wa kura ya        baraza kuu la HUDUMA chini ya uenyekiti wa Mwangalizi Mkuu wa HUDUMA, pasiwepo na      badiliko lolote wala kutoeleweka vizuri na pia kukubaliana kwa pamoja na kwa Sauti moja        tukimtukuza MUNGU na kujengana sisi kwa sisi na kufanya ushuhuda kwa Dunia.






Tarehe:……………………            Mwezi………………….…             Mwaka   …………………


……………………………………..                                                     ……………….…………………..
KATIBU MKUU                                                                                   MWENYEKITI

……………………………….………
MWEKA HAZINA
           















Sisi tulioorodhesha majina yetu hapa chini ni Washirika waanzilishi wa
MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA (M.M.M.T). Tunakubaliana na Masharti yaliyotajwa katika KATIBA hii na kwamba mabadiliko yoyote yanaweza kufanyika wakati wowote kwa makubaliano ya Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu.


NAMBA
JINA

WADHIFA
SAINI
1

BENJAMIN  LUCAS  MDOE
MWENYEKITI

2
FARAJA  BENJAMIN MDOE
MJUMBE

3
BLANDINA  DISMAS
MJUMBE

4
MICHAEL  KANYAWANA

MWEKA HAZINA

5
ROSE  MTANGO

KATIBU

6
ISLAEL  WILSON  KIULA

MJUMBE

7

JOHN  MGAYA
MJUMBE

8

JOSEPH   SIMON
MJUMBE

9
GRACE  MSABA

MJUMBE

10
ANNA  MOKIWA

MJUMBE



Maoni 7 :

  1. Katiba haionyeshi 1.Mgawanyo wa mapato. Kama zaka na Sadaka.
    2.Katiba haionyeshi Fedha itatunzwa wapi. Je,mtu za hazina atakuwa anazitunzia wapi?

    JibuFuta
  2. Hongereni Kwa katiba hiyo

    JibuFuta
  3. Maoni yangu Mimi nimugeni wa mazingira nasijasoma nauezo wakujisomesha sina nimetumwa kufufua kanisa lililofungwa nanimesha fufua tayari naomba naombamusaada rameck pct pefa kaguruka ngara kagera

    JibuFuta