Jumatatu, 26 Desemba 2016

DHAMIRA




DHAMIRA:

-Katika ufahamu (wa mtu) Mwanadamu kuna jambo fulani linalofanya kazi kama hakimu / wa maadili.Linawaambia watu mambo yaliyo mema na mabaya.Linawahimiza watu kufanya mema,nalo lina wahakikishia kama wamefanya mema au kama wana hatia,kufuatana na kutii au kutotii sauti hiyo ya ndani.Hakimu huyu wa maadili ndani yetu huitwa dhamiri.

 Kwa ufupi dhamiri ni ile hali ya kuona jambo au kusikia na  kufikiri yale unayofikiri na kutaka kuyatendea kazi./ dhamira inafanya kazi ya kupima na kuchuja na kisha kukuruhusu kufanya au kutenda. Unapofanya kwa wakati sahihi na mahali sahihi unapata amani na unapokosea unajisikia hukumu au hatia hiyo ndiyo kazi ya dhamira au kukukataza usifanye.
Rumi 2:15 – 16.”Hao waionyesha kazi ya torati iliyo andikwa moyoni mwao dhamiri yao ikiwashuhudia na mawazo yao wenyewe kwa wenyewe yakiwashitaki au kuwatetea; Katika siku ile Mungu atakapozihukumu,sawasawa na injili yangu kwa Kristo”.
1 Yohana 3:19-20 “Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wakweli nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake ikiwa miyoyo yetu inatuhukumu kwa maana Mungu ni mkuu kuliko miyo yetu, naye anajua yote.Wapenzi mioyo yetu isipo tuhukumu tuna ujasiri kwa Mungu”.

Katika agano la kaleinaeleza wazi inavyo fanya kazi. Mwanzo 3:7-8 “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa uchi wakashona majani ya mti wajifanyia nguo; Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu akitembea bustanini wakati wa jua. Kupunga Adamuna Mkewe wajificha kati ya miti ya bustani Bwana Mungu asiwaone. Kilichofanya Adamu na Mkewe wakajifiche. “Kilicho fanya Adamu na Mkewe wajifiche baada ya kusikia sauti ya Mungu ni ile hali ya dhamira ya mioyo yao ikiwaambia wamekosea na kujisikia hukumu.Kutokana na dhamira walijiona hawastahili kuonana na Mungu.
Ayubu 27:6 Haki yangunaishika sana wala sitaiacha.Moyo wangu hauta nisuta  wakatiniwapo hai. Dhamiri inajulisha makosa yako ungali bado uko hai na dhambi zako.
Daudi alijua makosa yake kwasababu dhamira ilimwambia.
Zaburi51:3-4 Maana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu imbele yangu daima. Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una, haki unenapo. Na kuwa safi utoapo hukumu.

-Kumbuka kuwa nia ni tofauti na dhamira lakini zinafanya kazi katika wakatimmoja.
-Mara nyingi watu wamekuwa wakipuuzia sauti ya ndani, matokeo yake wanajikuta wameangukia kwenye dhambina, baada ya hapo dhamira bado itasimama kuku hukumu. Kuwa umekosea unastahili adhabu.






JINSI GANI DHAMIRA INAWEZA KUFA / KUCHAFUKA:

 1.Kwa kutojali sauti ya dhamira inapo mshauri na kutoa hukumu. Nia inapo kataa ushauri na hukumu ya dhamira na kuamua kufanya kile nia inachoona / kusikia bila kujali kutatokea nini baada ya kutenda au kutotenda, mf.Kabla Adamu na Hawa hawaja muasi Mungu, nia pamoja na dhamira zilikuwa safi zilisikilizana.
Nia ilikubali kile dhamira inachosema. Dhamira ilisimamia kuwa muamuzi mzuri.
Hawa alipo kubali kumsikiliza shetani na kuruhusu msukumo mkubwa wa  nia ya shetani kugeuza nia yake,hatimae aliweza kupuuzia  Makatazo ya dhamiri bila kujali kutokea nini?
 Hapa ndipo dhamira ilipoanza kuharibika, unapoona mtu ana rudia-rudia dhambi hiyo mara kwa mara ujue dhamiri yake imekafa juu ya hukumu ya dhambi hiyo huona tu ni jambo la  kawaida kwake hata kama ataambiwa ni dhambi kwake yeye hakiri kuwa ni kosa.

 2. KUFA KWA DHAMIRA:

Dhamira inaweza kufa baada ya machafuko / kuchafuliwa bila kufanyiwa matengenezo ya usafi wa kweli wa kusikilizwa, na kufuta hatia zilizo moyoni; kwa damu ya Yesu Kristo. Mf. Tito 1:16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu bali kwa matendo yao wanamkana,ni wenye machukizo,waasi,wala kwa tendo jema hawafai.
Inafikia mtu analisoma Neno na anafanya tofauti na Neno na hajisikii hukumu. Kwa sababu dhamiri ilisha kufa kwa kutosikilizwa.

Kwa nini? Nia na dhamira kupingana? Nia na dhamiri hupingana kwasababu ya kukosa Neno ndani yake. Nia itafikiri sawa na Neno.Dhamira itahukumu sawa na Neno hapo hupata majibu yaliyo sahihi. Wakati mwingine dhamiri hupingana hapo mtu hujisikia kufanya jambo au kutofanya, kusita sita moyoni mwake.

DHAMIRA INAPO KUWA SAFI:

Dhamira iliyoendelea vizuri katika usafi humwongoza mtu ili ifanye mambo mema, haidhuru kama yameandikwa katika sheria fulani fulani au sivyo.
Rumi 13:5 Kwa hiyo ni lazima kutii. Si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamira, inafikia mahali tunaacha kufanya dhambi si kwasababu ya hukumu ya Mungu bali kwa sababu ya dhamiri safi ndani yetu ya kumpenda Mungu.
-Utaamua kwa busara na utafikiri kwa busara na kufanya kwa busara, bila upinzani.
1 Petro 3:16 Nanyi mwe na dhamiri njema. Ili katika Neno lile mnalosingiziwa.Watahayarishwe wale wautukanao Mwenendo wenu mwema katika Kristo.

FAIDA

Faida ya dhamiri na nia vikiwa, vime safishwa na kujaa Neno la Mungu.Utaweza kupambanua safi ya shetani na ya Mungu.
Kolosai 3:16 Neno la Kristo na likae  kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana. Kwa saburi na kwa nyimbo na tenzi za Rohoni huku mkimwimbia  Mungu kwa Neema Miyoyoni mwenu.
Maana yake kila matakalo kufanya lita kuwa sawa na Neno, na kila mtakalo tenda mtatenda sawa na Neno. Na kila mtakalosikia au kuona mtafanya sawa na Neno.
Kolosai 3:17 Nakila mfanyalo kwa Neno au kwa tendo, fanyeni yote kwa jina la Bwana Yesu, Mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

MAMBO YA KUTAMBUA: KATIKA KUWA SAFI; KATIKA DHAMIRI:-

  1. Kuna watu wanajisikia hukumu hata kama wametubu bado wanajisikia hawaja samehewa. Ni lazima waamini kuwa wamesamehewa, maana msamaha hutoka kwa njia ya imani kukiri mbele za Yesu na kuacha dhambi.
  2. Wajisamehe wao wenyewe binafsi kwa makosa waliyotenda katka nafsi zao na dhamiri zao. Kukiri na kuacha kujitendea nafsi zao mabaya.
  3. Waamini kuwa wamejisamehe na wao wamesamehewa la sivyo wataona hawaja samehewa, na pia ni ngumu kwao  kuwasamehe wengine. Na wao kupokea msamaha.
  4. Kama mwanadamu ni lazima utambue kwamba una dhamiri safi, si lazima kuwa bila kosa ishi kwa unyenyekevu hata kama  dhamiri yako ina kushuhudia huna kosa endelea kuishi maisha ya usafi, usijihesabie haki. 1.Kor 4:4 Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini nisi hesabiwe haki kwa ajili hiyo; Ila anihukumuye mimi ni Bwana.
  5. Dhamiri ni taa au jicho la kupambanua mema na mabaya, Kwa hiyo dhamiri yako inatakiwa kuwa safi Mbele ya Mungu wala siyo safi kwa kadiri ya taratibu au kanuni ambazo umejipangia mwenyewe.

-Dhamiri ikiwa chafu na mwili wako huwa mchafu / huwa giza. Luka 11:34 -36 Taa   ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga, lakini likiwa bovu mwili wako nao una giza. Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza. Basi kama mwaga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu liyo na giza mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikapo kwa mwanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni