Jumatano, 28 Desemba 2016
KUFANYIKA MAJIBU NINI?
Majibu nikutoa utatuzi wa tatizo lililopo au yaliyopo
Mfano tunapo kua na hitaji lamaji katika mjiwetu mtu
mmoja akajitolea kwafedha zake
kuchimba kisima na maji yakawa yana patikana kwamwaka mzima ingawa nikwafedha atakua amejibu tatizo lamaji kwake na watu wengine kitakacho bakia niwatu kutafuta fedha kwaajili yakununulia maji lakini siomaji haya patikani
Watu
wengi wana hangaika juu ya maisha yao kuwa ya shida yatabu ni kwa sababu hawaja amua kuijibu
dunia juu ya matatizo yake ISAYA 2:17-20
Hofu na shimo na mtego vijuu yako ewe
mwenye kukaa duniani itakua kila akimbiae
sauti ya hofu ataanguka katika
shimo nakila apandaye nakutoka
shimomoni atanaswa na mtego kwa maana madirisha yalio juu yamewekwa wazi
na misingi yadunia inatikisika
Kwajinsi hii
dunia inahitaji majibu katika
halizote dunia inamisingi mikubwa mine
(1)
Dini za
ulimwengu zimeshindwa kutoa majibu
ya kutosheleza kwa watu nazo zime pasuka maadili yame haribika
(2)
Msingi
wasiasa umepasuka wanasiasa ni waongo walarushwa mafisadi wauaji
(3)
Uchumi wa inchi
dunia kuwa ngumu watu wachache kuchukua ardhi nakuji limbikizia mali na kuficha fedha
(4)
Jeshi : haliya usalama wa inchi
na dunia sionzuri viongozi wana
salitiana kutaka madaraka watu kupinduana hivyo usalama
duniani nimdogo hivyo vyote
vina hitaji majibu
KUFANYIKA MAJIBU (A)TAMBUA WITO WAKO
Nivema kufahamu kuwa unatoa majibu
kwa watu ndivyo unavyopunguza matatizo
yako au ndivyo unavyo patamajibu
ya maisha yako au mahitaji yako
WITO NINI? Witoniile hali yakuitika
mguso wandani nakuufanya katika utendaji Mf Watoto waadamu
waliitika wito uliokua ndani yao
mmoja alijisikia kuwa mkulima na mwingine alijisikia kuwa mfugaji MWANZ 4:1-8 Ibrahimu aliitika wito wakutoka
ur-ya ukaldayo na kwenda kanani
mwanz 12:1-9 aliitika wito alio tumwa na mungu
AINA ZA WITO
Hakuna mtuasiye nawito hapa duniani isipokuwa inaweza ikawangumu
kujitambua ameitwa katika witogani
(1)wito wa mambo yakijamii :Rum 13:1-7 wito huu unahusu huduma zakijamii
na pia mungu anahusika katika wito huu ingawa wengi wana puuzia wanaona siokazi yamungu lakini nikazi ya Mungu ukifanya kwa
uaminifu nabidii Mungu anakubariki
(2)wito washughuli ambazo zina onekana
niza kawaida katika jamii kutoka31:1-3 kutoka 35:30 kwahiyo Mungu
aliwaita kwashughuli za kiufundi
(3)wito maalumu kwaajili yakazi ya Mungu Efeso 4:11 Mtume Manabii Wainjilisti Walimu
wachungaji
(4)Wito wa huduma ya masaidiano
kanisani wazee wa kanisa
mashemasi wahudumu waimbaji 1kori
12:28-29 mdo 6:1-5 huu niwito wamungu ana uheshimu na ukifanya kwabidii Mungu ana kubariki
Mtu anaweza kuwa nawito zaidi
yammoja napia watuwengine huzaliwa nao
kwaujumla wanao mpaka awepo mwenye ujuzi wakuibua
wito ulioko ndani ya mtu hivyo hujikuta
wapo wapo tu mpaka aonekane mwenye hekima
yakuwasaidia : mtu anajisikia kuimba
Lakini hajui kuimba huyuana hitaji mwenye elimu yakuimba,
amfundishe
KUFANYIKA MAJIBU :(B)MATUMAINI
YALIOKO KATIKA WITO
Matumaini
nini ?
Watuwengi wame katatamaa
kuendelea kukaa katika witowao kwa
Jumanne, 27 Desemba 2016
Jumatatu, 26 Desemba 2016
KATIBA YA KANISA
YALIYOMO
1.1. JINA LA HUDUMA
Jina
la huduma litakuwa “MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA”
Anuani ya huduma itakuwa
MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA
S.L.P 131.
HANDENI
TANGA
TANZANIA.
Makao makuu ya huduma hii yatakuwa
HANDENI - TANGA -
TANZANIA.
Tamko la Imani, kwa mwafaka na waumini wa agizo la
agano ( jipya) tunafungamana
na azimio la
tamko tuliaminilo yaani msingi wa Imani.(Yohana
3:16 )
Tukiombea kuwa kusiwe na madhara wala mgawanyiko
tofauti, na kudhuru amani miongoni mwa
Huduma ndani na nje ya nchi yamkini sote tudumu kwa haja moja, kwa upendo mmoja
kwa MUNGU mmoja mwenye enzi katika Imani zifuatazo:
(1Timotheo2:1-4.)
(a) Tunaamini kwamba Biblia ni kitabu kitakatifu
chenye sehemu mbili yaani Agano la Kale lenye vitabu
27 na Agano jipya lenye vitabu 39 ni neno lenye pumzi ya Mungu.Tunaifanya Biblia
kuwa na mamlaka ya mwisho kuhusiana na Tabia ya Mkiristo.
(2
Timotheo 3:16).
(b) Tuna
amini kwamba kuna MUNGU mmoja wa kweli, muumba wa mbingu na nchi na Yeso
Kristo ni mwana wake na Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu (1Yohana5:8-9).
(c) Tunaamini
katika wokovu kwamba mwanadamu anaweza kupokea wokovu kwa njia
ya Imani kwa kumuamini Mwana wa MUNGU YESU Kristo kupitia kazi nzito aliyoifanya
pale
Msalabani kwa msaada wa Roho Mtakatifu ( Warumi 10:9 ).
(d) (i)
Tunaamini kwamba Kanisa la kweli hujengwa chini ya Msingi wa Yesu Kristo ( 1 Wakorintho 3:11, Waefeso 2:20).
(ii)
Tunaamini kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo
(Warumi 12:5,Wakorintho12:2-15).na
(iii)
Tunaamini kwamba Kristo ni kichwa cha Kanisa
(Waefeso
5:23,Wakorintho11:3)
(e) Tunaamini katika ubatizo wa maji mengi.
Ubatizo wa maji mengi ni amri ambayo kila anayemwamini YESU ni lazima aitimize Amri
hiyo. YESU Kristo alituamuru tubatizwe katika
maji mengi.(Yohana 3:22-23, Warumi: 6:3-9).
(f) Tunaamini katika ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Ujazo wa Roho Mtakatifu ni ahadi kwa kila mwamini
ili kumwezesha mwamini kumtumikia MUNGU kwa Maombi na Kuabudu katika Roho
Mtakatifu (Matendo 2:4-11, Warumi 8:26, Waefeso 6:18).
(g)
Tunaamini katika huduma 5 yaani
Mitume, ManabÃi, Wainjilisti, Wachungaji na Walimu. (Waefeso 4:11-12).
(h)
Tunaamini ndoa ya mume na mke mmoja katika Kristo Bwana (Mathayo 19:3-
Malengo na Madhumuni ya HUDUMA
ni kama ifuatavyo:
(a) Kutekeleza
kiutendaji agizo la kupeleka na kusambaza Injili kamili ndani na nje ya nchi.
(b) Kufuata
mwangozo wa Roho Mtakatifu na kuandaa mfumo mzuri wa ushirikiano usio wa ubinafsi, na wenye maisha Matakatifu kwa
utendaji fanisi wa kazi ya MUNGU.
(c) Kutoa
uhuru wa kweli wa kuabudu na kutoa mafundisho thabiti katika Huduma na Washirika.
(d) Kudumisha
na kuleta ushirikiano na Huduma nyingine za kiroho.
(e) Kutoa
Huduma mbalimbali za Kiroho na Kimwili katika Jamii.
Kwa
mfano:
Kiroho:
Kufanya Semina na Mikutano ya Injili, Kuombea wagonjwa na
kuwapa Ushauri kwa
ridhaa yao mahospitalini, mashuleni,
magerezani na katika
kaya.
Kimwili:-
Kujenga
na kuendesha shule, Zahanati, Hospitali, na Karakana za ufundi, uchapishaji na Studio za
kureckodi uimbaji.
3.1.2.
Wachungaji wapya watapatikana kutokana na kukua kwa huduma, kipawa
huweza kutokea na kutunzwa kisha kuweza kuwekewa
mikono kuwa wachungaji na kusaidiwa kuanzisha
HUDUMA.
3.1.3. Wachungaji wanaojiunga
kutoka makanisa mengine kulingana na kutaka kutumia vipawa walivyopewa na Mungu kwa uhuru
zaidi.
3.3.3. Kutoa ushauri wa maono yake kwa lengo la
kusaidia, kuimarisha na kuendeleza malengo ya
HUDUMA, pamoja na michango ya hiari. Atapaswa kujiunga na mfuko wadharura
wa wachungaji.
3.4.1. Ana haki ya kupata huduma zote za kiroho na za kimwili kulingana na mazingira yake ya kazi (mfano chakula,
mahali pakuishi na matibabu yake) siyo malipo au mshahara.
3.4.3. Anapaswa
kutambua HUDUMA ni mali ya mahali pamoja, washirika pamoja na yeye na
siyo mali yake
ni mali ya Mungu.
na pia makao makuu ita husika
kumsaidia.
3.4.5. HUDUMA itaangalia familia ya mchungaji mpaka
pale watoto watakapo anza kujitegemea,
baada ya hapo HUDUMA ita
mlea mama na baba mchungaji, mpaka hapo Mungu atakapo wachukua.
3.4.6. Hata kama watakuwa wamepumzika kulingana na
umri watakuwa washauri wa wachungaji,
vijana, na watapaswa kuheshimiwa.
yeyote yule.
3.4.9. Hana haki ya kudai kurudishiwa michango
yoyote aliyotoa kwa hiari yake mwenywe kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za maendeleo ya HUDUMA.
3.5.5. Kutokana na kuasi
kwake atapaswa kuiacha huduma bali mali za kwake binafsi ataondoka nazo na mkewe akiendelea na imani aachwe
aendelee kuitunza hiyo huduma bali Baba hata tambuliwa.
Kutakuwepo na aina mbili za Washiriki nazo ni:
3.6.1. Washirika waanzilishi:
Washirika
hawa ndio walioshiriki katika kuandaa katiba hii.
3.6.1.Washirika wapya:
Washiriki
wapya wa huduma hii wataendelea kupatikana kutokana na Mikutano ya Injili,Semina, Makongamano na
Maombezi ya wagonjwa yatakayofanyika pamoja
na wenye shida mbalimbali.
(i) Awe ameokoka
(ii) Awe amebatizwa katika maji mengi
(iii) Awe anashiriki katika Ibada na semina za
Kiroho
(iv) Awe mwaminifu na mkwel kwa Mungu na kwa
jamii.i
(v) Awe anashiriki katika shughuli za Huduma kwa
kufuata taratibu zilizowekwa na zitakazo wekwa.
(i)
Kutekeleza maamuzi yote halali yatakayopangwa na HUDUMA kwa faida ya
HUDUMA.
(ii) Kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za
HUDUMA.
(iii) Kutoa ushauri utakaosaidia, kuimarisha na
kuendeleza malengo ya
HUDUMA.
(i) Anahaki ya kupata huduma zote za Kiroho mfano
maombi, huduma
za ndoa, mazishi, ugonjwa, ushauri nasaha na
unasihi.
(ii) Anahaki ya kuhoji anapoona dalili za
ubadhilifu wa mali za HUDUMA.
(iii) Hana haki ya kudai kurudishiwa michango ya
aina yoyote aliyotoa kwa hiari yake mwenyewe kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za maendeleo ya HUDUMA.
(iv) Anao uamuzi wa kuendelea au kutoendelea na
huduma bila kubughuziwa na mtu yoyote yule.
(v) Ana haki ya kuilinda na kuitetea misingi ya
imani ya Kikristo.
Kikomo cha mshirika katika HUDUMA kitasababishwa na :-
(i)
Kufukuzwa kwa kushindwa kufuata kanuni za Imani, Taratibu na Sheria zilizowekwa na HUDUMA.
(ii)
Anapoamua kuacha kuwa Mshirika kwa hiari yake mwenyewe.
Muundo wa serikali kuu ya HUDUMA
itakuwa kama ifuatavyo:
Kutakuwa na:-
(i)
Mwangalizi Mkuu.
(ii) Katibu Mkuu.
(iii)
Mweka Hazina.
(iv) Wangalizi wa Kanda
(v)
Wangalizi wa Majimbo.
(vi)
Wasimamizi wa Vituo vya HUDUMA
(vii) Wazee na Watumishi wa Vituo vya HUDUMA.
Ni mwiko kwa Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa
kutumia madaraka aliyopewa kwa ajili ya manufaa yake
binafsi au kuwa na upendeleo wa namna yoyote ambao ni kinyume na zilizowekwa.
Katika uchaguzi wowote ule kiongozi atakuwa ni yule
atakayepata zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa na wajumbe
wanao husika waliohudhuria katika uchaguzi huo.
Kutakuwa na Baraza kuu la
Serikali ya HUDUMA. Baraza hilo litaundwa na Wajumbe wafuatao.
4.2.1.
Kamati kuu Tendaji.
4.2.3.
Baraza la Waangalizi wa Kanda na Majimbo.
4.2.4.
Wasimamizi wa Vituo vyote vya HUDUMA katika majimbo.
4.2.5.
WazeeViongozi wa Vituo vya HUDUMA katika
majimbo
4.2.6 Wakuu wa Idara zote
katika HUDUMA
4.2.7.
Wajumbe waalikwa / wataalamu.
Baraza kuu litakuwa na kazi zifuatazo:
4.3.1. Litakuwa na mamlaka ya
kuteua, kuchagua, kusimika, kusimamia utendaji kazi na kutengua nyadhifa zao itakapo bidi.
4.3.2.
Litasimamia shughuli zote za HUDUMA.
4.3.3. Litasimamia maadili ya
watumishi wote wa HUDUMA kwa ujumla.
4.3.4. Baraza kuu
litakutana mara moja kila mwaka kati ya mwezi Desemba na Januari na
maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.
4.3.5. Litasimamia mali zote
4.3.6.
Kurekebisha katiba ya huduma itakapohitajika kufanyiwa marekebisho.
4.3.7. Kupitisha taarifa za maendeleo ya huduma na
kutoa mwongozo mpya.
Wafuatao watakuwa ni Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji:
4.4.1. Mwangalizi Mkuu wa HUDUMA.
4.4.2. Katibu Mkuu.
4.4.3. Mtunza Hazina.
4.4.5. Wangalizi wa Kanda.
4.4.6. Wazee wa HUDUMA 2 wateuliwa.
Majukumu ya Kamati Kuu Tendaji yatakuwa kama
ifuatavyo:
4.5.1. Itafanya na kusimamia shughuli za
kila siku za utendaji wa
HUDUMA.
4.5.2. Itatoa mapendekezo yatakayo jadiliwa
na kupitishwa na Mkutano wa
Baraza kuu.
4.5.3. Hakuna kikao cha Kamati Kuu
Tendaji kitakachofanywa bila
kuwepo na
koramu ya wajumbe wapatao theluthi mbili( 2/3).
4.5.6. Kurekebisha katiba ya huduma itakayo
hitajika kufanyiwa marekebisho
4.5.7. Kupitia taarifa za
maendeleo ya huduma na kutoa miongozo mipya.
Mwangalizi Mkuu Atachaguliwa na Baraza kuu la Waangalizi.
Majukumu ya Mwangalizi Mkuu yatakuwa kama
ifuatavyo:-
5.1.1. Atakuwa na
mamlaka ya kuangalia kazi zote za HUDUMA Kitaifa.
5.1.2. Atawajibika
kufuatilia utendaji wa kazi wa Wangalizi wote walioko chini yake.
5.1.3. Atakuwa
mwenyekiti wa Mikutano yote ya Baraza kuu na Kamati Tendaji.
5.2.1. Awe na Ujuzi katika Shughuli
zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
5.2.2. Awe na Elimu ya
Sekondari na kuendelea.
5.2.3.
Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau cheti)
5.2.4. Awe mtu
asiyelaumika katika Jamii(Timotheo3:1-7)
5.2.5.
Awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza kwa lugha fasaha yaani Kiswahili, Kiingereza.
5.3.1. Katibu Mkuu atapendekezwa na Kamati Kuu
Tendaji na atapitishwa na Baraza kuu.
5.3.2.
Atakuwa katika Utumishi huu kwa muda wa miaka 5.
5.3.3. Kulingana na uwezo wake wa utendaji
anaweza kuteuliwa tena.
5.4.1. Awe na ujuzi wa kazi zitakazofanywa na
HUDUMA si chini ya miaka 5.
5.4.2
Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea
5.4.3. Awe na Elimu ya
chuo cha Biblia (angalau cheti)
5.5.0. MAJUKUMU YA KATIBU MKUU:
5.5.1.
Atawajibika katika Utawala na Kuendesha Kazi za HUDUMA chini ya
Usimamizi wa Mwangalizi Mkuu
5.6.2. Atatunza kumbukumbu
zote za Wasimamizi wa Vituo vya HUDUMA na taarifa zote za Uongozi.
5. 5.3. Atakuwa katibu katika vikao / mikutano
yote ya Baraza kuu na Kamati utendaji
5.6.1. Mtunza Hazina atapendekezwa na Kamati
Kuu Tendaji na atapitishwa na Baraza kuu.
5.6.2 Atakuwa katika Utumishi huu kwa muda wa miaka
5.
5.6.3
Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu wake katika HUDUMA anaweza kuteuliwa tena.
5.7.1. Awe Mshirika wa Huduma.
5.7.2.
Awe na Elimu ya Kidato cha 4 na kuendelea.
5.7.3. Awe na Taaluma ya Uhasibu.
5.7.4. Awe mwaminifu na aliyejitoa kikamilifu kwa
MUNGU.
5.8.1. Atawajibika katika utunzaji na ukaguzi wa
mali na fedha zote za Huduma.
5.8.2. Atatayarisha Taarifa ya Fedha, Mapato
na Matumizi na kuwasilisha mbele ya Baraza Kuu.
5.8.3. Atatekeleza kazi
zake kwa kushirikiana na viongozi wake pamoja na Watumishi wengine wa HUDUMA hasa Mwangalizi
Mkuu na Katibu Mkuu.
Mwangalizi wa Kanda atachaguliwa na waangalizi wa
Majimbo wa kanda husika na kithibitishwa
na Baraza kuu.
6.1.1. Awe na Ujuzi
katika Shughuli zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
6.1.2. Awe na Elimu ya
Sekondari na kuendelea.
6.1.3. Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau
cheti)
6.1.4. Awe mtu asiyelaumika katika Jamii(Timoteo 3:1-7)
Kulingana na uweza wa utendaji na uaminifu
wake katika HUDUMA anweza kuteuliwa tena.
6.2.1 Atawajibika kihuduma katika maeneo yote ya
Kanda yake.
6.2.2. Atawajibika kufuatilia utendaji wa kazi ya
Mungu katika majimbo ya kanda yake.
6.2.3. Atakuwa
mwenyekiti wa mikutano na vikao vyote vya majimbo yake.
6.3.0.
UTEUZI WA MWAGALIZI WA JIMBO/WILAYA:
6.3.1. Mwangalizi
wa Jimbo/Wilaya atachaguliwa na Kamati
Tendaji na
Kuthibitishwa na Baraza kuu
6.3.2. Atatumika chini ya usimamizi wa mwangalizi wa
kanda
6.3.3.
Kipindi cha utumishi kitakuwa miaka 5.
6.3.4. Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu
wake katika HUDUMA anaweza
kuteuliwa
tena
6.4.1. Awe
na Ujuzi katika Shughuli zitakazofanywa na HUDUMA si chini ya miaka 5.
6.4.2. Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.
6.4.3. Awe na Elimu ya Chuo cha Biblia(angalau
cheti)
6.4.4.
Awe mtu asiyelaumika katika Jamii (Timotheo3:1-7)
6.4.5. Awe mtu mwenye uwezo
wa kujieleza kwa lugha fasaha yaani
Kiswahili, Kiingereza.
6.5.1. Atawajibika
kihuduma katika maeneo yote ya Jimbo / Wilaya yake.
6.5.2. Atawajibika kufuatilia
utendaji wa kazi ya Mungu katika makanisa yaliyo ndani ya jimbo lake / wilaya.
6.5.3. Kulingana na uwezo wa utendaji na uaminifu
wake katika HUDUMA anaweza
kuteuliwa tena.
6.6.1. Msimamizi wa kituo cha HUDUMA atateuliwa kulingana na
Wito na Vipawa vya MUNGU vilivyo ndani mwake na kuthibitishwa
na Mwangalizi Mkuu.
6.6.2. Msimamizi wa Kituo Cha
HUDUMA atatumika chini ya usimamizi wa Mwangalizi wa Majimbo/Wilaya.
6.7.1. Atawajibika kihuduma katika Kituo cha HUDUMA
anacho kiongoza kwa heshma na utumishi wake mzuri.
6.7.2. Atapaswa apewe heshima sawa sawa na huduma ya
kazi yake.
6.7.3.
Atateua viongozi katika Kituo chake, kuwasimika na kutengua
nyadhifa zao itakapo bidi.
6.7.4. Atawajibika kulea vipawa mbalimbali vitakavyo
ibuka katika Kituo Chake
6.7.5.
Anatakiwa awe na uwezo wa kuongoza Washirika. (Ezekieli 23:4, 6, 15, 34:1-3,
Matendo 20:28, Yohana21:15-17,1Petro
5:1-2)
6.7.6. Anapaswa awe mtumishi
mkweli na mwaminifu kwa MUNGU na kwa
jamii.
6.7.7. Anao wajibu wa
kulinda na kutunza mali
za Kituo cha HUDUMA anacho kiongoza.
Washirika wote wa HUDUMA hii wanawajibika kwa
kuzingatia Mwongozo na sheria, pia kuwa
na nidhamu, yamkini wanastahili adhabu wakifanya
uhalifu wowote ule.
Wazee na Wasimamizi wasaidizi wa Kituo cha HUDUMA -
Watateuliwa na kusimikwa na Msimamizi
wa kituo cha HUDUMA. na watatumika chini ya uongozi wake.
8.1.1. Awe ameokoka.
8.1.2. Awe amebatizwa katika
maji mengi.
8.1.3. Awe mwaminifu na mkweli kwa Mungu na
kwa jamii.
8.2.1. Wanawajibika kumsaidia MSIMAMIZI WA KITUO
CHA HUDUMA
8.2.2. Kutoa ushauri kwa msimamizi wa kituo na washarika kwa ujumla.
8.3.0. IDARA ZA HUDUMA:
8.3.1. Idara ya Uinjilisti.
8.3.2.
Idara ya Vijana
8.3.3.
Idara ya Muziki
8.3.6. Idara ya Wanawake na Watoto.
8.3.7. Idara ya Akinababa.
Idara zote
katika kila kituo cha HUDUMA zitateuliwa na MSIMAMIZI WA KITUO CHA HUDUMA HUSIKA.
Kipindi cha huduma kitakuwa ni
miaka mitatu ( 3 ).baada ya hapo wakiwa hawana
lawama
zozote
wanaweza kuendelea tena kipindi kingine.
Katika kila ngazi
ya juu ya uongozi kutakuwa na msaidizi atakaefanya kazi za kiongozi mkuu atakapokuwa
na udhuru.
Baraza
kuu litakutana mara moja kila mwaka kati ya mwezi Desemba na Januari.
Kutokana na miradi
mbalimbali / shughuli za kuogeza kipato.
Kutakuwa na matoleo ya aina mbalimbali, mfano
sadaka za hiari, minada ya vitu mbalimbali na
harambee.
Kutakuwa
na miradi mbalimbali ya HUDUMA
Mfano: KILIMO, KARAKANA, STUDIO, VITUO VYA
REDIO, SHULE, TV,USAFIRI,HOSPITALI, UCHAPAJI
NA UUZAJI VITABU.
Mapato yote yatakayopatikana yatatumika katika
shughuli za maendeleo ya HUDUMA yakifuata
taratibu zote za kiuhasibu, lengo likiwa ni kufanikisha kuipeleka Injili
ya BWANA katika Nchi yote ya Tanzania na nchi nyingine pia. Aidha sehemu ya
mapato itatumika kutoa huduma ya kiroho na za kimwili katika jamii.
Mfano:- Kutoa huduma za kuwatunza
yatima, wajane na masikini.
Baraza la wadhamini litateuliwa na baraza
kuu. Wajumbe wake hawatakuwa zaidi ya 5 na si chini ya watatu. Hawa watawajibika kulinda mali zote za HUDUMA.
Huduma
ya mdhamini itaisha endapo kutatokea:
9.1 Kifo
9.2 Kujiuzulu
9.3 Kura ya kutokuwa na Imani na mjumbe kutokana
na mkutano wa wadhamini.
9.4 Mdhamini atatumikia wadhifa huu katika
kipindi cha miaka 5.
9.5 Vikao vya wadhamini vitaendeshwa kwa kura ya
wingi wa korumu isiyopungua wajumbe 3.
Baraza la wadhamini litakutana mara
mbili kwa mwaka.
Kipengele
hiki kimewekwa ili kurekebisha au kupendekeza marekebisho ya kanuni ama
sheria ya katiba hii. Pendekezo la
marekebisho litafikishwa kwenye baraza kuu kwa uthibitisho.
Katiba inaweza kufanyiwa marekebisho kwa Koramu ya
theluthi mbili 2/3 za wingi wa kura ya baraza
kuu la HUDUMA chini ya uenyekiti wa Mwangalizi Mkuu wa HUDUMA, pasiwepo na badiliko lolote wala kutoeleweka vizuri na
pia kukubaliana kwa pamoja na kwa Sauti moja tukimtukuza
MUNGU na kujengana sisi kwa sisi na kufanya ushuhuda kwa Dunia.
Tarehe:…………………… Mwezi………………….… Mwaka …………………
…………………………………….. ……………….…………………..
KATIBU MKUU
MWENYEKITI
……………………………….………
MWEKA HAZINA
Sisi
tulioorodhesha majina yetu hapa chini ni Washirika waanzilishi wa
MJI WA MAKAIMBILIO MINISTRY TANZANIA (M.M.M.T). Tunakubaliana na Masharti yaliyotajwa katika KATIBA
hii na kwamba mabadiliko yoyote yanaweza kufanyika wakati wowote kwa
makubaliano ya Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu.
NAMBA
|
JINA
|
WADHIFA
|
SAINI
|
1
|
BENJAMIN
LUCAS MDOE
|
MWENYEKITI
|
|
2
|
FARAJA
BENJAMIN MDOE
|
MJUMBE
|
|
3
|
BLANDINA
DISMAS
|
MJUMBE
|
|
4
|
MICHAEL
KANYAWANA
|
MWEKA HAZINA
|
|
5
|
ROSE
MTANGO
|
KATIBU
|
|
6
|
ISLAEL
WILSON KIULA
|
MJUMBE
|
|
7
|
JOHN MGAYA
|
MJUMBE
|
|
8
|
JOSEPH
SIMON
|
MJUMBE
|
|
9
|
GRACE
MSABA
|
MJUMBE
|
|
10
|
ANNA
MOKIWA
|
MJUMBE
|
|
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)