NGUVU YA MAOMBI |
NGUVU YA MAOMBI
Utangulizi.
kitabu hiki kizima cha matendo kimegawanywa katika mambo matatu : (1) juu (2) chini
(3)nje.
Ikiwa na maana Yesu alipaa juu. Roho mtakatifu alishuka chini kanisa
lilikwenda nje kabla hawajaenda ulimwenguni yesu aliwapa Amri nyingine , Hii inaitwa Amri kuu mdo 1:4 yesu aliwaambia mwahitaji kwanza kwaenda kwenye mukutano wa maombi (mstari 8) lakini
mtapokea nguvu ili akisha kuwajilia juu
yenu Roho mtakatifu , nanyi mtakuwa
mashahidi wangu hata mwisho wa
nchi , Tunaona katika 1wakor 15:6 yesu
aliwapa amri hii watu miatano 500
lakini wanafunzi 120 tu ndio walio tii
wanafunzi 380 walishindwa kutii lina maanisha
76% au 3 kati 4, walifanya kitu kugine
wengi wetu tunajua umuhimu wa maombi jinsi ulivyo. Lakini hatufanyi kimatendo.
Uhusiano
kati ya uinjilisti ulimwenguni na maombi uwezo wa kubadilisha kwa kupitia maombi: Yesu aliunganisha
maombi na mavuno ya Roho za watu
zilizopotea mathayo 9: 35-38,marko 16:15.Tatizo Mavuno ni
mengi lakini watenda kazi ni wachache
mathayo 9:37.ufumbuzi , mathayo 9:38 muombeni
bwana wa mavuno.
Uhusiano
kati ya umoja wa kikristo na maombi : uwezo wa kubadilisha kanisa maombi ni
muhimu kwa sababu yana leta hali ya
umoja kanisani mdo 4:31-32)
kuongezeka kwa maombi kuna ashiria kuongezeka kwa umoja .
uhusiano kati ya kukua kibinafsi na
maombi .maombi yanatufanya tukue kiroho. Mitume walianzisha kipaumbele hiki cha huduma :Maombi na huduma ya neno matemdo 6:4. Haiwezekani kukua
kufikia uwezo wetu katika kristo bila
maombi (yuda 20) lengo la kwanza la maombi ni kumjua kristo yesu zaidi kuliko
kumjua mtu mwingine ni lazima utumie muda wako na mtu Yule wafilipi 3:10)
Maombi
ni
nini? Ni ushirikiano na
asiyeonekana na aliye mtakatifu”.
maana nne za
maombi kama zilivyoelezwa (1)
maombi ni kuomba nguvu ya kirohikimaanisha,maombi ni kumuita mungu wakati wahitaji ni kumuomba mungu kwa ajili ya
Baraka au nguvu ili tuweze
kukua kwake na kwamba tuweze kuhudumiwa
mahitaji yetu. (2) Maombi yanafanya
shughuli za kiroho.Yaani maombi ni kuingia katika mapatano na mungu kuondoa
vipingamizi vya shetani wakati mwingine tuombapo kile kisicho cha kawaida kinatokea,Hatuombi mungu afanyekitu badala yake kwa mamlaka ya jina la Yesu tunaamuru mlima kung’oka.Hii inaitwa sheria ya mamlaka ya
ikroho mathayo 16:19,18:18-19) .
(1)Maombi ni kupokea siri za kiroho :Ni kumsikiliza
mungu ni kumruhusu mungu atuambie siri
zake kwa hiyo maombi nikuongea na mungu
kuhusu mambo ya ndani ni kusema “Roho
mtakatifu ni hakusikia: Daneli 2:21-22. (3) maombi ni kuendeleza upendo wa
kiroho kwa hiyo inatubidi tufikiri juu
ya maombi kama jambo la upendo binafsi na Baba aliye mbinguni kwa
kupitia Yesu kristo. Umuhimu wa maombi: maombi
huchangia kukua kwetu kiroho ikimaanisha kama siombi sikui
maombi huchangia nguvu yetu ya kiroho . ikimaanisha nguvu ya kiroho inamaanisha na nguvu ya siku kwa siku
tunayohitaji kutoka kwa bwana. Maombi huchangia msimamo wetu kiroho.Hapa
panahusu sifa zile za uaminifu ambazo zinatusaidia kuwa thabiti
kwa yesu.
Mpango
au ratiba ya maombi: Mambo mawili ya
muhimu katika kuwa na mpango wa maombi .Maombi yetu yawe ya
utaratibu na maanisha kuwa na
mpango kufanya kitu kwa mbinu au mathubuti. Pia wakati wa maombi
uwe ume andaliwa yaani .Tuwe na vitu tofauti tofauti ambavyo tunatazamia
.Ayubu13:18. Pia wakati wa maombi yetu uwe dhahiri (mathayo 7:7
)maombi yetu yawe makamilifu kwa hii tuna maanisha kwamba
inatubidi kujumuisha yale yote ambayo ni maombi wakati tunapoomba .katika ujumbe unaotuambia kuhusu vita vya kiroho Efeso6:18. Mathayo 26:40-41.
Mazoezi
ya maombi zipo njia 12 dhahiri za kibiblia za kuomba: (a) kusifu nini Ni kumwinua mungu nikumheshimu kwa maneno
ambayo yanatangaza jinsi alivyo
zaburi 63:3) (b) kukaa kimya :Roho ya
kimya ni kukaa kimya ni kumpenda mungu na kuwa makini kwa mungu
zaburi 46:10 (c)kuungama ni
kumruhusu mungu kusafisha hekalu
letu kutokana na dhambi
zaburi 139: 23. (d) Kuomba kwa maandiko ,Hii ni kudai maneno ya maandiko
katika maandiko katika maombi yeremia 23:29.(e)kukesha:Hii ni kuendeleza kuwa
macho kitakatifu katika maombi yetu kolosai 4:2.Hii ni kuchukua dakika
chache kufikiri kuhusu jambo ambalo ni
ngeombea, mahitaji ambayo Roho mtakatifu
ataleta kwenye akili yangu.
F) maombezi,hii ni kuombea wengine ,ni kupigana vita vya kiroho kwa ajili yaw engine kwa kuchukua
mahitaji yao mbele ya mungu au kwa kushindana na shetani kwa niaba yao (1
timoth 2:1-2)
G) Maombi ya mahitaji. Hii ni kuleta mahitaji
yangu binafsi mbele ya Mungu kwa maombi yote viwili kiroho na kimwil.
H) Shukurani. Hii ni
aina ya kukiri na kusema asante katika maombi shukurani ni kusema asante kwa
jili ya jambo ambalo amekutendea, 1 thesa 5:18).
(i) Kuimba ni kufanya tuni
katika maombi,
(j) Kutafakari: Hii ni aina nyingine ya maombi ya
kuwa kimya, kutafakari na kufikiri kiroho katika maombi .Yoshuo 1:8,
K) Kusikiliza: Huku ni
kumsikiliza mungu katika maombi.
(L) kusheherekea: ni
kufurahia kwa shangwe katika maombi
.Tulianza maombi kwa kumuinua mungu na sasa tunafunga kwa maombi na muda wa kumfurahia mungu aliyo mwaminifu kwa
kuitikia maombi yetu .kusudi la
maombi ni kusaidia kukusanya katika
mavuno Roho zilizopotea. Mathayo 24:14
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni