Jumapili, 29 Januari 2017

NGUVU YA MAOMBI

NGUVU YA MAOMBI


 NGUVU YA MAOMBI

Utangulizi. kitabu hiki kizima cha matendo kimegawanywa katika mambo matatu : (1) juu (2) chini  (3)nje.  Ikiwa na maana Yesu alipaa juu. Roho mtakatifu alishuka chini kanisa lilikwenda nje  kabla hawajaenda  ulimwenguni yesu aliwapa Amri  nyingine , Hii inaitwa Amri kuu mdo 1:4  yesu aliwaambia mwahitaji  kwanza kwaenda   kwenye mukutano wa maombi (mstari 8) lakini mtapokea nguvu ili akisha  kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu , nanyi mtakuwa  mashahidi  wangu hata mwisho wa nchi , Tunaona katika  1wakor 15:6 yesu aliwapa amri hii watu miatano  500 lakini  wanafunzi 120 tu ndio walio tii wanafunzi 380 walishindwa  kutii lina maanisha 76% au  3 kati 4, walifanya kitu kugine wengi wetu tunajua umuhimu wa maombi jinsi ulivyo. Lakini hatufanyi kimatendo.
   Uhusiano kati ya uinjilisti ulimwenguni na maombi uwezo wa kubadilisha kwa kupitia maombi: Yesu aliunganisha maombi na mavuno ya Roho za watu  zilizopotea  mathayo  9: 35-38,marko 16:15.Tatizo Mavuno ni mengi  lakini watenda kazi ni wachache mathayo 9:37.ufumbuzi , mathayo 9:38 muombeni  bwana wa mavuno.
 Uhusiano kati ya umoja wa kikristo na maombi : uwezo wa kubadilisha kanisa maombi ni muhimu kwa sababu yana leta  hali ya umoja  kanisani  mdo 4:31-32)  kuongezeka  kwa maombi  kuna ashiria kuongezeka kwa umoja . uhusiano  kati ya kukua kibinafsi na maombi .maombi yanatufanya tukue kiroho. Mitume walianzisha kipaumbele  hiki cha huduma :Maombi na huduma  ya neno matemdo 6:4. Haiwezekani kukua kufikia uwezo wetu katika  kristo bila maombi (yuda 20) lengo la kwanza la maombi ni kumjua kristo yesu zaidi kuliko kumjua mtu mwingine ni lazima utumie muda wako na mtu Yule wafilipi 3:10)
Maombi ni nini?  Ni ushirikiano  na  asiyeonekana na  aliye mtakatifu”. maana  nne za maombi kama zilivyoelezwa (1) maombi ni kuomba nguvu ya kirohikimaanisha,maombi ni kumuita mungu  wakati wahitaji ni kumuomba mungu  kwa ajili ya  Baraka au  nguvu ili tuweze kukua  kwake na kwamba tuweze kuhudumiwa mahitaji yetu.  (2) Maombi yanafanya shughuli za kiroho.Yaani maombi ni kuingia katika mapatano na mungu kuondoa vipingamizi vya shetani wakati mwingine tuombapo kile kisicho  cha kawaida kinatokea,Hatuombi  mungu afanyekitu badala yake kwa  mamlaka ya jina la Yesu  tunaamuru mlima kung’oka.Hii  inaitwa sheria ya mamlaka ya ikroho mathayo 16:19,18:18-19) .
(1)Maombi  ni kupokea siri za kiroho :Ni kumsikiliza mungu  ni kumruhusu mungu atuambie siri zake kwa hiyo  maombi nikuongea na mungu kuhusu mambo ya ndani ni kusema “Roho mtakatifu ni hakusikia: Daneli 2:21-22. (3) maombi ni kuendeleza upendo wa kiroho  kwa hiyo inatubidi tufikiri juu ya maombi  kama jambo la  upendo binafsi na Baba aliye mbinguni kwa kupitia Yesu kristo. Umuhimu  wa maombi:  maombi  huchangia kukua kwetu kiroho ikimaanisha kama siombi  sikui  maombi  huchangia nguvu  yetu ya kiroho . ikimaanisha nguvu ya  kiroho inamaanisha na nguvu ya siku kwa siku tunayohitaji kutoka kwa bwana.  Maombi  huchangia msimamo wetu kiroho.Hapa panahusu  sifa  zile za uaminifu ambazo zinatusaidia  kuwa thabiti  kwa yesu.
  Mpango au ratiba ya maombi: Mambo mawili  ya muhimu  katika kuwa na mpango wa maombi .Maombi yetu yawe ya utaratibu  na maanisha kuwa na mpango  kufanya kitu  kwa mbinu au mathubuti. Pia wakati wa maombi uwe ume andaliwa yaani .Tuwe na vitu tofauti tofauti ambavyo tunatazamia .Ayubu13:18.  Pia wakati  wa maombi yetu uwe dhahiri (mathayo 7:7 )maombi yetu yawe makamilifu kwa hii tuna maanisha  kwamba  inatubidi kujumuisha yale yote ambayo ni maombi wakati  tunapoomba .katika ujumbe  unaotuambia kuhusu  vita vya kiroho Efeso6:18. Mathayo 26:40-41.
Mazoezi ya maombi  zipo njia 12 dhahiri za kibiblia za kuomba:  (a) kusifu nini   Ni kumwinua mungu  nikumheshimu kwa  maneno  ambayo   yanatangaza jinsi alivyo zaburi 63:3)  (b) kukaa kimya :Roho ya kimya ni  kukaa  kimya ni kumpenda mungu na kuwa makini  kwa mungu  zaburi 46:10 (c)kuungama  ni kumruhusu mungu kusafisha  hekalu letu  kutokana  na dhambi  zaburi 139: 23. (d) Kuomba kwa maandiko ,Hii ni kudai maneno ya maandiko katika maandiko katika maombi yeremia 23:29.(e)kukesha:Hii ni kuendeleza kuwa macho  kitakatifu  katika maombi yetu  kolosai 4:2.Hii ni kuchukua dakika chache  kufikiri kuhusu jambo ambalo ni ngeombea, mahitaji  ambayo Roho mtakatifu ataleta kwenye akili yangu.
F)   maombezi,hii ni kuombea  wengine ,ni kupigana vita vya  kiroho kwa ajili yaw engine kwa kuchukua mahitaji yao mbele ya mungu au kwa kushindana na shetani kwa niaba yao (1 timoth 2:1-2)
 G) Maombi ya mahitaji. Hii ni kuleta mahitaji yangu binafsi mbele ya Mungu kwa maombi yote viwili kiroho na kimwil.
H) Shukurani. Hii ni aina ya kukiri na kusema asante katika maombi shukurani ni kusema asante kwa jili ya jambo ambalo amekutendea, 1 thesa 5:18).
(i) Kuimba ni kufanya tuni katika maombi,
(j)  Kutafakari: Hii ni aina nyingine ya maombi ya kuwa kimya, kutafakari na kufikiri kiroho katika maombi .Yoshuo 1:8,
K) Kusikiliza: Huku ni kumsikiliza mungu katika maombi.
(L) kusheherekea: ni kufurahia kwa shangwe katika  maombi .Tulianza maombi kwa kumuinua mungu na sasa tunafunga kwa maombi na muda  wa kumfurahia mungu aliyo mwaminifu kwa kuitikia maombi yetu  .kusudi la maombi  ni kusaidia kukusanya katika mavuno  Roho zilizopotea. Mathayo 24:14


MISINGI YA IMANI

Utangulizi : Fundisho hili msingi wa imani lili fundishwa kwa  lengo la kuimalisha washirika  wapya kwenye masomo ya misingi na mafundisho haya maalumu ya msingi yameweza kugawangwa katika vipengele sita na kufundishwa kwa wazi kabisa kama ifuatavyo.
            Biblia ni neno la Mungu.
Hapa Biblia ilielezwa wazi kuwa Biblia maana yake ni kitabu na inavitabu sitini na sita vilivyo andikwa kama Barua ,Historia,Masimulizi,Mashairi,Tenzi na Matukio ya mwisho yote hayo yakiwa na maudhui ya nayo fanana. Na Mungu alihariri kitabu hiki kwa zaidi ya miaka1500-1400.kabla ya kristo hadi  mwaka wa 100 B.K na waandishi wake ni arobaini 40, wamo Wachungaji  wakuki Mashujaawa vita ,Makasisi,Manabii,Wafalme ,Madaktari wan tiba ,wasomi na wahudumu .Kila kizazi ,Kila utamaduni taifa na kila kabila laweza kupona kwa hiyo tumethibitisha kuwa Biblia ni neon la Mungu tungika kwa maana. Biblia ili vuviwa na Mungu  .Biblia ndiiyo kanuni na mwongozo wetu wa maisha ,Biblia ni kitabu cha mawazo ya Mungu hukupatia yote unayohitaji kwa maisha ya kiroho na maendeleo ya mkristo ( 2petro 1:20-21 isaya 55:7-11, 1petro 2:2 . Mathayo 4:4,
Utatu Mungu mmoja aliye aliyejidhihirisha katka nafasi tau. Biblea imeeleza kuwa Mungu tunaye mwamini sisi wakristo ni mmoja aliye jidhihirish katika nafsi tatu kumb 6:4, Mwanzo 1:26 wakati wa uumbaji alisema natufanye. (Mwanzo 1:26), Mungu amejitaja katika wingi (mwanzo 11:6-7) utatu una maanisha (mathayo 28:19) (a) Mungu Baba (b) Mungu mwana, (1) Mungu Roho mtakatifu na biblia inataja kuwa hao wote watatu ni Mungu. Yohana 1:1, 14 Y esu ni Mungu (2) Roho mtakatifu ni mungu
Mdo 5:3-4)
   Uungu wa Yesu. hapa biblia imeeleza kuwa yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa na Bikira mariamu. Mith 30:4 Baba yake Yesu ni Mungu na Yesu ni zaidi ya mtu mwema. Nabii na Yesu Mwenyewe ni Mungu. Maana alijiita niko Yohana 8:57-58 kwa hiyo kiini cha ukristo ni Uungu wa yesu. Utume wa Yesu.
 Utume wa Yesu alikuja ulimwenguni kwa vile mwanadamu alitengwa na Mungu kwa sababu ya kuanguka katika dhambi  kama wanadamu hatuna uwezo wowote wakujikomboa wenyewe kwa hiyo ukristo ni pale Mungu anapo wafikia wanadamu  chini kwa hiyo Mungu ana jitambulisha pamoja na wanadamu Kwahiyo Yesu alikuja Duniani kutoa uhai wake kama dhabihu kwa wanadamu . Ilikutuleta kwa Mungu 1kor 15:21-22) Wokovu kwa neema kwa njia ya Imani Mungu, Jehanamu na kurudi kwa kristo, Yesu hutoa wokovu kwa neema kwa njia ya imani Efeso 2:8-9.
Lazima tuupokee wokovu bure kwa kufanya Toba. Toba hutangulia imani  (Makro 1:15 Toba ni msamaha wa dhambi (matendo 2:36-38 kwa hiyo toba ni  mabadiliko ya moyoni yanayo tokeza mabadiliko ya nje na tabia kwa hiyo kila mtu anayezaliwa ,mara ya pili hufanyika mshirika wa kanisa la kristo liitwalo mwili wa kristo Mbingu na jehanamu .
 Jehanamu ni sehemu ya moto na mateso jehanamu ilitayarishwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake na sio wafu na wale wanaomkataa kristo Yesu kipawa chake cha bure cha wokovu wataenda jehanamu .Na hakuna anae weza kutoroka jehanamu baada ya kufika huko na haiwezekani kubadilimawazo baada ya kufa na jehanamu ni sehemu inayo inayo tunza moto (ziwala moto) Mbingu inawasubiri wale watakao kuwa wamempokea Yesu Moyoni mwao.
Kurudi kwa Yesu  , Biblia inaeleza kurudi kwa Yesu kutawala na Mungu mwisho atajenga mbingu mpya na nchi mpya , uf 21:1,10-11                                                                                                                                                                                                                                                     luka 16:22-26  Roho mtakatifu ni nafsi Yohana 14:15-18 Yesu alitoa ahadi kumtuma Roho mtakatifu iliawe nasi  na kufanya kazi ya kristo .
Ubatizo wa Roho mtakatifu                                                                                                                                                                                                                                         mtakatifu ni tukio linalo linalo fuata wokovu na linalo patikana kwa kila mtoto wa Mungu .Aina mbili za ujuzi wa Roho mtakatifu alizo fundisha Yesu (1). Ubatizo  yohana 4:13-14 (2) Ubatizo wa Roho mtakatifu yohana  7:37-39) Uponyaji wa kiungu:  Mungu anajifunua kwa watu wake kama mponyaji  kutoka  15:23-26) Jehova Rapha .Ni bwana atuponyae Mungu huponya mwili pamoja na nafsi msamaha –Roho ,Mwili =Mgonjwa ,Uponyaji sehemu ya kazi  ya Ukombozi wa kristo manabii walitabili uponyaji huu wa kimwili na kiroho .Isaya 53:1-5